HUDUMA ZA MATIBABU KISARAWE KUWA BORA ZAIDI
Posted on: October 1st, 2019Hospitali ya Wilaya ya Kisarawe inategemea kuboresha huduma za Mama na Mtoto kupitia Ujenzi wa Jengo lenye Gorofa moja ambalo limeshaanza kujengwa Hospitalini hapo.
Akizungumza hospitalini hapo Mganga mfawidhi wa Hospitali hiyo Dr. Yonah J. Kabata alisema huduma katika Hospitali hiyo itaboreka zaidi baada kukamilika kwa Jengo hilo.



